HUYU HAPA MZAWA KUPEWA MIKOBA YA KAZE NDANI YA YANGA

Imeelezwa  kuwa baada ya Cedric Kaze raia wa Burundi kufutwa kazi ndani ya kikosi hicho mikoba yake atakabidhiwa mzawa Juma Mwambusi ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Mwambusi alijiweka kando ndani ya Yanga kutokana na kile ambacho alieleza kwamba hakuwa kwenye afya bora na alishauriwa  ajitenge na kazi ambazo zitahusisha kelele ama kuzungumza kwa muda mrefu.

Baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar akiwa na Kaze, Mwambusi aliomba kujiweka kando na Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla alithibitisha suala hilo.

Hivi karibuni Mwambusi alisema kuwa yupo fiti kiafya baada ya kurejea kwenye ubora wake jambo ambalo linatoa nafasi kwake kurejea kwenye majukumu ya kufundisha.

"Kwa sasa ninaendelea salama na nipo sawa hivyo nina amini kwamba ninaweza kurejea kwenye majukumu yangu hali itakapokuwa sawa kwa asilimia 100," alisema.

Kwa sasa Yanga haina benchi la ufundi baada ya Kaze kufutwa kazi Machi 7 baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma 1-1 na kufanya timu hiyo kugawana pointi mojamoja na Polisi Tanzania.

Ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 50 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo ilianza mzunguko wa kwanza ikiwa na Mwambusi pamoja na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ambaye naye alifutwa kazi.

Kesho timu inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi mzunguko wa pili.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments