KOCHA AWAAMBIA YANGA KUNA KIONGOZI ANAWAHUJUMU

Aliyekuwa kocha wa magolikipa wa Klabu ya Yanga, Mrundi, Vladmir Niyonkuru amefunguka mambo mengi baada ya benchi la ufundi la klabu hiyo kuvunjwa siku ya 7 Machi 2021 kufuatia mwenendo wa matokeo yasiyoridhisha kwa viongozi na wanachama wa timu hiyo.

 

Akizungumzia namna benchi hilo lilivyoondolewa, Niyonkuru amesema; “Hawajatuitisha sisi kwa pamoja, kila mtu aliitwa kivyake. Mimi wakaniambia wakiangalia timu inavyoenda kwa sasa, tumeamua tusitishe mkataba na wewe. Mimi sikuuliiza zaidi sababu ila niliwapa mkono na kushukuru na nikaondoka zangu.

 

 Baada ya kusema hayo, kocha huyo aliyejiunga na Yanga mwezi Agosti mwaka jana, aligusia juu ya moja ya kiongozi anayeiharibu timu hiyo ikiwemo kuingiliwa kwenye majukumu yao kama benchi la ufundi.

 

Mimi siwezi kumtaja huyo tu lakini yupo, alijaribu kufanya hivyo. Nawaambia Wanayanga na mashabiki wake wakiwa wanachagua viongozi, wachague viongozi walio sahihi.


Maelezo yake hayo yaliendelea na hata kukiri kuwa kuna kiongozi anayeiharibu timu huyo ila hayupo tayari kumtaja.

 

Nakwambia kuna kitu, kuna kitu kipo nyuma na kuna mtu ana haribu hiyo timu ninyi waandishi mfanye uchunguzi mtajua.”

 

 Maneno hayo yamezidi kuwaaminisha wadau wa soka nchini kuwa, kwenye Uongozi wa Klabu ya Yanga kuna mapungufu mengi baina ya viongozi wa juu jambo linalochangia timu hiyo kukosa utulivu hivi sasa na kupelekea kupata matokeo mabaya. 


Benchi lote la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze lilivunjwa na kwa sasa timu ipo mikononi mwa Juma Mwambusi.


Post a Comment

0 Comments