Recent-Post

MSUVA: AWATUMIA UJUMBE SIMBA, NAMUNGO

Mshambuliaji  wa timu taifa ya Tanzania na klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco, Saimon Msuva amesema kuwa anaamini klabu za Namungo na Simba zina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kama tu watapambana.

Namungo juzi Jumatano walipoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi D la michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0, kutoka kwa Raja Casablanca ya nchini Morroco, huku Simba wao wakiwa wanaongoza kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumzia nafasi Namungo kwenye michuano hiyo Msuva amesema: Nimekuwa niwafuatilia kwa ukaribu mkubwa wawakilishi wa Tanzania Kimataifa, Simba  na Namungo kwa upande wangu naamini timu hizi zitafanya vizuri endapo tu zitapambana mwanzo mpaka mwisho.

Namungo wanatakiwa wasijione kuwa ni wageni wakashindwa kufanya vizuri, mpira ni ule ule muhimu ni kupambana kwani wana wachezaji wazuri ambao wanaweza kuipa mafanikio timu hiyo, pia niwapongeze kwa hatua ambayo wamefikia

Post a Comment

0 Comments