Recent-Post

TOTTENHAM WAJIPANGA KUMPATA MRITHI WA HUGO

Imelipotiwa kuwa Klabu ya Tottenham inampigia hesabu kipa wa Manchester United, Dean Henderson ili kurithi mikoba ya kipa wao Hugo LIOris.

Sababu kubwa za timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England kuwa kwenye hesabu za kumpata kipa mpya ni kwamba kipa wao ana mpango wa kuondoka England na anahitaji kwenda kucheza nyumbai kwao nchini Ufaransa.

Mkataba wake ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho unakaribia kufika ukingoni msimu huu jambo ambalo linaongeza nguvu kwa Tottenham kusaka mbadala wake.

Henderson mwenye miaka 24 anatengenezwa ndani ya United kuwa mrithi wa David de Gea ambaye amepewa chaguo la kufanya maamuzi anayotaka ndani ya timu hiyo kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa ni kumpa heshima ya utumishi wake ndani ya kikosi hicho kwani naye anahitaji kuondoka pia.

LIoris alijiunga na timu ya Tottenham msimu wa 2012 na amecheza jumla ya mechi 363 mkataba wake unameguka msimu huu.


Post a Comment

0 Comments