TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAKUTANA NA WADAU KUJADILI TAARIFA YA MAPENDEKEZO YALIYOTOLEWA NA BARAZA LA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI

 


 

TUME ya Haki za Binadamu na utawala bora nchini imekutana na wadau  wa Idara,Taasisi na Wizara mbalimbali za Serikali Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na Baraza la haki za Binadamu Duniani kuhusiana na maendeleo ya masuala ya haki za binadamu.

 

Akizungumza katika kikao cha kujadili taarifa hiyo,jana jijini hapa Mwenyekiti wa Tume hiyo,Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa Tanzania kama nchi mwanachama wa Baraza hilo la haki za binadamu hutakiwa kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kama ushauri  kuhusiana na masuala ya maendeleo ya haki za binadamu.

 

Amesema baraza hilo huwa linajishuhulisha na masuala ya haki za binadamu kwa nchi wanachama na Tanzania kama wanachama huhitajika kupleka taarifa kuhusiana na maendeleo ya haki za binadamu

 

Jaji Mwaimu amesema kuwa kutokana na mapendekezo hayo  ambayo yapo 227yaliyotolewa na Baraza hilo la haki za binadamu  kwa  Tanzania kama mwanachama ambayo iliyakataa baadhi ya mapendekezo takribani 93yalitolewa na Baraza hilo mwaka 2016 ambapo mawili wameyatekeleza ikiwemo mfumo wa utoaji haki,masuala ya haki za walemavu pamoja na kuboresha kuhusu kuboresha masuala ya utekelezaji akina mama  kiuchumi.

Amesema kila baada ya miaka minne wamekuwa wakituma taarifa ya maendeleo ya haki za binadamu ambapo ifikapo Machi25 mwaka huu Tanzania itapeleka taarifa hiyo makao makuu ya Baraza la haki za binadamu nchini Geneva Uswiss.

“Tumeandaa taarifa ya Tume yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu hivyo kila mwaka baraza hufanya kikao na kutoa mapendekezo kwa nchi wanachama ili kuyatekeleza,”alisema

Amesema maeneneo mengine ambayo hawajayaweka katika taarifa hiyo ambayo ina kurasa tano watachagua yale ya muhimu na kupokea ushauri na kuyaboresha mapendekezo hayo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo,Muhamed Hamisi Hamad amesema kuwa taarifa hiyo ya haki za binadamu inahusu Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wamechukua hatua mbalimbali zimefanyika ikiwemo haki za wanawake ikiwemo uteuzi wa nafasi za wanawake katika uongozi

Kuna masuala mbalimbali ya haki za kijamii na kiuchumi zimefikiwa ikiwemo maji,afya kwa makundi mbalimbali ambapo utekelezaji wake umepiga hatua.

Naye Kamishina Paul Masanja wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema kuwa Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa na wadau wa haki za binadamu wanawajibika kutoa ripoti kwa Baraza hilo ili kuonyesha kama hayo yanafanyika nchini

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments