UKARABATI WA MTO LUKOSI RUAHA MBUYUNI WAKAMILIKA

 Na. Mwandishi wetu; Ruaha Mbuyuni – Iringa

Ukarabati wa kingo za Mto Lukosi uliyopo katika Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, unayopeleka Maji yake katika mto Ruaha mkuu na kutumika katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni, umekamilika baada ya kusombwa na mafuriko makubwa yalitokea mwaka jana, yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika ukanda wa nyada za nyanda za juu kusini.

Mtambo aina ya Excavator ukifanya kazi ya kuiinua tuta kwa kupanga mawe katika mto Lukosi, ili kuurejesha katika njia yake ya asili.


Akizungumza baada ya kukamilika kwa kazi hiyo Mhandishi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Daniel Manase alisema mafuriko hayo yaliyoharibu kingo yenye urefu wa takribani mita 180, yalisababisha kingo za mto kubomoka na hivyo mto kuacha njia ya asili na kuanza kupita kwenye mkondo mpya uliojitokeza.

Aliongeza kwa kusema kuwa, Kuhama kwa mto kulipelekea banio la skimu ya Umwagiliaji Ruaha Mbuyuni kukosa maji na mazao yaliyokuwa shambani yalikauka, Mhandisi Manase Alisema, baada ya kufika katika eneo hilo na kuona hali alisi kazi kubwa ilikuwa ni kutengeneza barabara ya muda kwanza ili kuweza kufika katika eneo lilikoharibika kutokana na mazingira kutokuwa rafiki.

Alisema, Kazi ya ujenzi iliendelea kwa kujaza mawe na vifusi katika ujenzi wa tuta ili kulimmarisha. “Pamoja na kwamba tulikuwa na vifaa vetu, tulipata msaada wa nyongeza ya eskaveta, kutoka kwa muwekezaji Kilimanjaro express anayefanya uwekezaji katika maeneo hayo, na kufanya kazi usiku na mchana karibia masaa 29, ili kuweza kuzunguka na kuziba gema maana maji yalikuwa yanakula gema.” Alibainisha.



“Tulizunguka kwa umbali wa kilometa 25 ili kuweza kubeba mawe na vifusi kuhakikisha kazi inakamilika, mwanzoni tulikuwa tunazunguka umbali wa kilomita tano kutokana na kwamba hali haikuwa nzuri ikabidi tuzunguke hizo kilomita 25.” Alisisitiza Mhandisi Manase.

Mhandisi Manase alisema, Kazi ya kupandisha tuta ilikuwa na changamoto ya mvua kutokana na kwamba vifaa vilikuwepo, magari yaliyokuwa yakikwama yalikwamuliwa.

Mhandisi Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Daniel Manase akizungumzia kuhusu kazi ya kurejesha Mto Lukosi katika njia yake asili, Ruaha Mbuyuni Mkoani Iringa.

Aliendelea kusema kuwa kwa sasa kazi hiyo imekamilika na wananchi katika maeneo hayo wanaweza kuendelea na shughuli za kilimo katika skimu ya Ruaha mbuyuni kama kawaida kwani hali ya mazingira sasa imesharudi katika hali yake ya kawaida.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments