SAFU ya ulinzi ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imeweza kuweka rekodi ya kuwa ni namba moja kwa kuruhusu mabao machache.
Simba imefungwa mabao 9 ambayo ni machache kwa timu zilizo ndani ya tatu bora, ipo nafasi ya pili, Yanga ipo nafasi ya kwanza, ukuta wake unashika namba mbili kwa kuokota mabao mengi ambayo ni 14.
Ukuta wa Simba unaongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ambao wamekuwa na maelewano makubwa na ni chaguo la kwanza kwa Gomes.
Ukuta wa Yanga ulianza kuwa na maelewano mwanzo wa msimu ila kwa sasa taratibu uimara umeanza kumeguka chini ya Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.
Azam FC iliyo nafasi ya tatu ukuta wake ni namba tatu kwa kuokota mabao mengi ikiwa imeruhusu mabao 17 katika mechi 24 msimu wa 2020/21. Kiongozi wake ni Yakub Mohamed.
0 Comments