Recent-Post

WAKALI WA PASI ZA MWISHO, LUHENDE NI NAMBA MOJA KWA WAZAWA


 WAKATI kukiwa na vita ya kuwania kiatu cha ufungaji ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambacho kipo mikononi mwa Meddie Kager, kuna vita pia ya utengenezaji mipango.

Kwa sasa Kagere yeye anatunishiana misuli na mshikaji wake John Bocco ambao wote wapo ndani ya Simba na wamefunga mabao 9.

Anayewafuata kwa ukaribu ni Prince Dube wa Azam FC mwenye mabao 8 ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Kwa upande wa watengeneza mipango ambao wao kazi yao ni kutoa pasi za mabao, Clatous Chama na Luis Miquissone wa Simba wanaongoza wakiwa wametoa jumla ya pasi 9.

Anafuata mzawa, David Luhende wa Kagera Sugar akiwa ametoa jumla ya pasi 7 ni namba moja kwa wazawa wenye pasi nyingi msimu wa 2020/21.

Pia Dube yeye ana pasi tano huku Yacouba Songne akiwa na jumla ya pasi nne ndani ya Yanga.

Post a Comment

0 Comments