Recent-Post

Walioshambuliwa na wanyama walilia kifuta machozi

Sengerema. Wananchi Wilaya ya Sengerema wamelalamikia idara ya wanyapori kutokuwalipa kifuta machozi watu waliopoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya kuliwa na wanyama wakali tangu mwaka 2019 hadi mwaka 2020.

Mmoja wa waathiriwa hao, Sanda Deus anayeishi Kijiji cha Nyamasale kata ya Busisi Wilayani humo aliyejeruhiwa mguu na mamba wakati anaogelea ziwa Victoria  Agosti 17, 2020 amelalamika kutokupa kifuta machozi hadi Sasa.

Amesema licha  ya taarifa zake kufikishwa idara ya Maliasili wilaya ya Sengerema tangu alipopata dhahama hiyo hadi sasa hajapata chochote.

“Tunaziomba mamlaka husika zitusaidie ili tupate kifuta machozi," amesema  Deus alipozuingumza na Mwananchi wilayani humo.

Ofisa Maliasili wilayani humo, Paul  Pontian amesema tangu mwaka 2019 hadi mwaka 2020, watu watano wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba na mmoja amejeruhiwa huku mbuzi 12 na kondoo 3 wameliwa na fisi.

Amesema taarifa hizi amekwisha zifikisha ofisi ya wanyamapori Kanda ya Ziwa nab ado anasubiri taratibu za malipo ya watu hao.

Post a Comment

0 Comments