WATANO WA YANGA KUIKOSA COASTAL UNION MKWAKWANI

Ikiwa kesho inatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkwakwani kusaka pointi tatu mbele ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union, Yanga inatarajiwa kukosa huduma ya nyota wake watano.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa moja ya jambo ambalo limetibua mipango yake ni pamoja na kadi nyekundu ya Carlos Carlinhos raia wa Angola.

Nyota huyo atakosa mchezo wa kesho Machi 4 kwa kuwa alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kosa la kumpiga ngumi beki wa Ken Gold, Boniphace Mwanjonde dakika ya 80.

Mbali na huyo pia Saido Ntibanzokiza yupo zake nchini Burundi ambapo alikwenda kwa ajili ya maandalizi ya timu yake ya Taifa ya Burundi baada ya kuitwa.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya alikuwa tayari ameanza kuingia kwenye mfumo na uwezo wake kwenye mechi dhidi yake dhidi ya Ihefu, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons uliweza kuonekana.

Mwingine ni beki wa kati Dickson Job ambaye yeye bado hajawa fiti kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja licha ya kuanza mazoezi mepesi.

Kiungo Mapinduzi Balama, bado hali yakehaijatengamaa na ameanza naye pia mazoezi mepesi. 

Kipa namba tatu wa Yanga, Ramadhani Kabwili hayupo fiti.

Kaze amesema:"Carlinhos alianza kurejea kwenye ubora wake kwa kuwa alikuwa nje ya uwanja akitibu majeraha sasa amepona anaingia kwenye mtego wa kadi, hamna namna tutatafuta mbadala wake,".

Post a Comment

0 Comments