Moshi. Mkazi wa Kata ya Marangu Mashariki wilayani hapa, Baltazari Mtui anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaunguza makalio watoto wake wawili wa kiume.
Inadaiwa kuwa baba huyo aliweka panga kwenye moto kisha akawaunguza watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili katika Shule ya Msingi Lyasongoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alithibitisha kutokea tukio hilo Aprili 16, mwaka huu.
Alisema wanamshikilia Mtui kwa kosa la kujeruhi na kwamba, taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Ni kweli tukio hili lipo na bahati nzuri mtuhumiwa amekamatwa na kesi inaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani,” alisema Kamanda Kakwale.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyasongoro, Jackson Mkonyi alisema, “walichofanyiwa na baba yao inaonekana si mara ya kwanza, wameteswa kwa muda mrefu, baada ya kupigiwa simu na msamaria mwema kunieleza wanavyofanyiwa ukatili kwa kuchomwa kwenye makalio na panga lenye moto, nilikwenda hadi nyumbani kwao kuwaona, nilipowachunguza na kuwakagua kwa kweli walikuwa wameumizwa vibaya sehemu za makalioni.
0 Comments