Recent-Post

ISHU YA SIMBA KUFUNGIWA KISA KWASI NA FIFA BARUA IPO HIVI


Imeelezwa kuwa Simba imepewa muda wa kukamilisha malipo ya mchezaji wao wa zamani, Asante Kwasi ambaye alipeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka Duniani, (Fifa) ili kupata stahiki zake.

Kwa mujibu wa barua ambayo waliandikiwa Simba kutoka Shirikisho la Soka la  mpira la Ghana, PfaG liliwaeleza kuwa wanapaswa kumlipa mchezaji huyo stahiki zake baada ya kushinda rufaa.

Barua hiyo iliandikwa Februari 26,2021 zama za Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha ambaye kwa sasa ni Mshauri wa Kuelekea kwenye Mabadiliko ndani ya Yanga.

Maamuzi ya Fifa yalifanyika awali Januari 15,2020 na pia shauri la pili likatolewa maamuzi Februri 2021 baada ya mchezaji huyo kukata rufaa.

Fifa iliwaambia Simba kwamba wanapaswa kulipa kiasi cha USD 4,000 kwa ajili ya malipo ya stahiki za mchezaji Kwasi ambaye alicheza Simba akitokea Klabu ya Lipuli. 

Habari zimeeleza kuwa Simba wamepewa muda kukamilisha malipo ya mchezaji huyo ambaye msimu wa 2017 alicheza Lipuli akitokea Klabu ya Mbao na aliachwa Simba msimu wa 2019 

Habari kutoka uongozi wa Simba zimeeleza kuwa bado hawajapata taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments