MATOLA ATUMA SALAMU YANGA HATUSHUKI KILELENI

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola ameibuka na kutoa kauli ya kibabe kwa wapinzani wao kwamba watakachokifanya ni kutotoka katika nafasi ya kwanza waliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara hadi watwae ubingwa. 

 Matola ameongeza kwamba kitu kikubwa ambacho wanachokifanya kwa sasa ni kupambana kwenye mechi zao kwa kushinda kwa ajili ya kufanikisha azimio lao la kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu huu.

 Kabla ya mechi ya jana, Simba wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 58, moja mbele ya wapinzani wao Yanga ambao wana pointi 57.

 Matola ameliambia Championi Jumatano,kwamba kwa sasa plani yao ni kushinda mechi hizo ikiwemo zile za viporo kwa ajili ya kuendelea kukaa kileleni. 

 Mipango yetu kwa sasa ni kukaa kileleni na hatutashuka hadi tunachukua ubingwa wakati msimu ukiisha. 

 Sisi tungekaa kwenye nafasi hii muda mrefu lakini mechi zetu za kimataifa zilikuwa zinatuchelewesha na kusababisha tuwe na viporo.

 Kwa sasa tutapambana tusitoke tena hadi mwisho wa msimu katika nafasi ambayo tupo na tutahakikisha mechi zetu zote ambazo ziko mbele tunashinda,” alimaliza

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments