Recent-Post

Nape ahoji kina Halima Mdee kuendelea na ubunge licha ya kufukuzwa Chadema

 napepic

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2021/2022, jijinin Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amehoji sababu ya Bunge kuendelea kuwatambua wabunge 19 wa viti maalum waliofukuzwa Chadema na kutaka uamuzi wa chama hicho kuheshimiwa.

Wabunge wa  hao wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee walifukuzwa kwenye chama hicho Novemba 27, 2021  baada ya kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa bila idhini ya Chadema.

Hata hivyo, walikata rufaa Baraza Kuu la Chadema kupinga kufukuzwa lakini mpaka leo hawajasikilizwa.

Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa Chadema ni Ester Bulaya, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Hawa Mwaifunga, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Salome Makamba na Jesca Kishoa.

Wengine ni Tunza Malapo, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Conchesta Rwamlaza, Cecilia Pareso, Agnesta Lambert, Asia Mohammed, Stella Fiao na Felister Njau.

Akizungumza jana Ijumaa Aprili 23, 2021 katika mdahalo uliowahusisha viongozi wa vyama vya siasa ulioendeshwa kupitia mtandao wa Zoom, Nape amesema suala hilo liko wazi kwamba hawastahili kuwa wabunge kwa mujibu wa katiba.

Post a Comment

0 Comments