Dodoma. Wabunge nchini Tanzania wameitaka Serikali ifanye jitihada za ziada katika kuhakikisha changamoto za kifedha na za kikodi zinazolalamikiwa na wananchi wa pande zote mbili za Muungano, zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Jana Makamo wa Rais Dk Philip Mpango wakati akifungua kongamano la miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bila kuzitaja alisema changamoto 15 kati ya 25 za muungano zilitatuliwa.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Joseph Mhagama ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 27, 2021 wakati akitoa maoni yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira.
Amesema kamati inaendelea kushauri Serikali ifanye jitihada za ziada katika kuhakikisha changamoto za kifedha na za kikodi zinazolalamikiwa na wananchi wa pande zote mbili za Muungano, zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Amesema hatua ambayo itachochea ukuaji wa uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na kwa manufaa ya Serikali zote mbili.
Aidha, Serikali iendelee na juhudi hizo katika kubaini changamoto mpya zinazoweza kuibuka na kuzitatua kwa haraka.
0 Comments