Recent-Post

LAMINE AWEKWA MTU KATI YANGA KISA NIDHAMU

 

MABOSI wa Yanga Jumatano walimuita nahodha wa timu hiyo, Mghana, Lamine Moro kwa kwa ajili ya kusikiliza shauri lake la utovu wa nidhamu.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu beki huyo aondolewe kambini huko Ruangwa, Lindi wakati Yanga ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC kutokana na ishu ya utovu wa nidhamu.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, CPA, Haji Mfikirwa, alisema wamechukua maamuzi ya kumuita beki huyo na kufanya naye kikao baada ya kupata malalamiko kutoka benchi la ufundi kwa ajili ya kusikiliza upande wa pili kabla ya kutenda haki kwa kutoa maamuzi.


“Benchi la Ufundi limelalamika, na kwa nafasi yao walichukua hatua za awali zilizopo kwenye mamlaka yao, kwa kuwa wamelileta kwa uongozi, sasa ni muhimu tukamsikiliza mlalamikiwa kisha kutoa maamuzi kama klabu.

 

“Suala la Lamine ni la kinidhamu lililoanzia kwenye bechi la ufundi na halihusiani chochote na kuidai klabu na kwamba mchezaji huyo hana deni lolote analoidai klabu kwa mujibu wa makubaliano," .

 

Lamine pia alikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 na kusepa na pointi tatu muhimu.

 

Post a Comment

0 Comments