Recent-Post

MANCHESTER CITY INA MPANGO NA STERLING

 

MANCHESTER City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola ina mpango wa kumuongezea mkataba nyota wao Raheem Sterling msimu huu kwa ajili ya kuwa naye msimu ujao na dili ambalo anatarajiwa kupewa ni kubwa.

Sterling alijiunga na City mwaka 2015 akitokea Klabu ya Liverpool inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp ambaye kwa sasa anapambana kuona timu yake inamaliza ndani ya nne bora.

City wana matumaini makubwa ya kupata huduma ya nyota huyo ndani ya Uwanja wa Etihad msimu ujao kwa kuwa amekuwa na maelewano na wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

Mshambuliaji huyo amekuwa ni chachu ya mafanikio ya timu hiyo ambapo amenyanyua mataji matano ya Ligi Kuu England na msimu uliopita alitupia  jumla ya mabao 10 na msimu huu pia amefunga mabao 10 na pasi saba.

Post a Comment

0 Comments