Recent-Post

YANGA WATOA MSAADA DODOMA

 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa sababu kubwa ya kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji ni kurudisha shukrani kwa jamii.

Jana, Mei 20 uongozi wa Yanga uliweza kutembelea shule ya watoto yatima iitwayo Zamzam iliyopo Dodoma mjini na kupata fursa ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika shule hiyo.

Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa maamuzi ya kufanya hivyo ni kurudisha kidogo wanachokipata kutoka kwao.

"Ambacho tumekifanya Dodoma ni kwa ajili ya kurudisha kile ambacho kidogo tumekipata kutoka kwao.

"Tunatambua sana mchango wao na tumeamua kuwapa kidogo ambacho tumepata ili waweze kuendelea kuwa na furaha na kutuunga mkono mara kwa mara tutakapokuwa Dodoma," amesema. 

Yanga ilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzaia uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ampabo ilishinda kwa mabao 2-0 na kufikisha jumla ya pointi 61 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo

Post a Comment

0 Comments