Recent-Post

KIUNGO AMBUNDO: NITACHEZA YANGA

Kiungo wa Dodoma Jiji, Dickson Ambundo amesema kuwa hana mashaka na uwezo wake ikiwa atapata dili la kucheza ndani ya Yanga kwa kuwa kazi yake ni mpira hivyo ana imani anaweza kucheza ndani ya timu hiyo pamoja na timu nyingine.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye mabao matatu na pasi nne za mabao amekuwa akitajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi raia wa Tunisia ambao wanatajwa kuhitaji saini yake.

Ambundo amesema kuwa anaskia habari zake za kuhitajika na Yanga jambo ambalo bado halijafika mezani kwakwe ila anaamini ana uwezo wa kucheza.

Ninaweza kucheza Yanga kwa kuwa uwezo wangu upo wazi na kazi yangu ni mpira hivyo sina mashaka na uwezo wangu jambo lolote linaweza kutokea ikiwa nitapata nafasi.

Kikubwa ambacho wanatakiwa kufanya Yanga kama wananihitaji ni kufuata utaratibu kwa kuzungumza na viongozi wangu ili waweze kukamilisha taratibu za usajili,” amesema Ambundo. 

Chanzo: Championi

Post a Comment

0 Comments