Rais Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro


Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro, ambako Wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu hivi karibuni.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.

Amesema amesikitishwa na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa Wafanyabiashara hao, na kwamba kama ingekuwa ni lazima Wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza uamuzi huo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan,  Wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya  kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments