Askofu Gwajima, Silaa kuhojiwa kamati ya maadili ya Bunge

 

Dodoma. Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima pamoja na Mbunge wa Ukonga (CCM) Jerry Silaa wameitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 21, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Bunge, imeeleza wabunge hao wameitwa mbele ya Kamati hiyo kwa agizo la Spika wa Bunge Job Ndugai.

Soma zaidi:Bunge latoa ufafanuzi kuhusu zuio kwa wabunge ambao hawajapata chanjo ya corona


“Wanatakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 4 (1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Juni 2020 ambayo inaipa mamlaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza mambo yanayohusu maadili ya wabunge yanayopelekwa na Spika” imesema taarifa hiyo.


Hata hivyo taarifa imeeleza kuwa, Mbunge Gwajima anatakiwa kufika kwenye Kamati hiyo siku ya Jumatatu Agosti 23, 2021 saa saba mchana na Mbunge Silaa anatakiwa kufika Jumanne Agosti 24 saa saba kamili mchana.


“Yeyote kati ya waliotajwa hatafika mbele ya Kamati kwa siku na muda uliotajwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa kifungu cha 17 na 34 (1) (a)  cha sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge, Sura ya 296, Toleo la mwaka 2020” imesema taarifa hiyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments