AZAM WAKWEA PIPA KUIBUKIA ZAMBIA

 BAADA ya kukamulisha ishu ya usajili, utambulisho wa nembo mpya, utambulisho wa uzi mpya pamoja na slogan mpya Azam FC leo wamekwea pipa kuelekea Zambia.



Ni Edward Manyama aliyekuwa anakipiga ndani ya Ruvu Shooting ambaye ni nyota pia ndani ya timu ya taifa ya Tanzania,  taifa Stars ni miongoni mwa waliotambulishwa.


Nembo yao mpya ilizinduliwa na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari,  Innocent Bashungwa ambaye alikiri kwamba ni nembo bora.


Kwa upande wa slogan mpya wanakwenda na mwendo wa kimyakimya. Leo wamekwea pipa kuibukia Zambia.


Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC,  Abdulkalim Amin amesema kuwa watakuwa na maandalizi mazuri yatakayowafanya wapate matokeo chanya.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments