BIASHARA WAANZA KUJIWINDA KIMATAIFA

 

KIKOSI cha Biashara United kutokea mkoani Mara, kinaendelea na mazoezi mazito ya kujiandaa na msimu ujao wa 2021/22, huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo ya hatua ya awali ya kombe la Shirikisho Afrika.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Biashara United imepangwa kuanzia ugenini na FC Dikhil ya Djibout kati ya Septemba 10 hadi 12, ambapo iwapo itafanikiwa kupenya katika michezo yao miwili ya awali, inatarajiwa kuvaana na mshindi baina ya Hay Al-Wadi ya Sudan, na Ahli Tripoli ya Libya.

Biashara United imepata nafasi hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita ambapo walikusanya pointi 50 katika michezo yao 34 waliyocheza, hivyo wataungana na Azam kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo.

Akizungumzia maandalizi yao kiungo wa Biashara United, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ amesema: “Tayari tumeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa 2021/22 chini ya kocha mkuu, Patrick Odhiambo, ambapo tageti yetu kubwa ni kuhakikisha tunafika mbali kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

“Kocha wetu anayafahamu vizuri mashindano haya hivyo amekuwa akituandaa kuendana na uhitaji tulionao.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments