Gwajima alikuja kwa dharau na kejeli - Mbunge CCM


 Mbunge wa Kilindi (CCM) nchini Tanzania, Omary Kigua amesema ujio wa Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu shauri lake la kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge ulikuwa wa dharau na kejeli.

Kigua ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 31, 2021 wakati akichangia katika ripoti ya kamati hiyo kuhusu shauri la mbunge huyo.

Soma hapa: Askofu Gwajima ahojiwa akiwa amesimama Kamati ya Bunge

Amesema wameshuhudia vituko katika kamati hiyo na kwamba vitendo vya mbunge huyo havifanani na nafasi aliyonayo katika Bunge.

Soma hapa: Askofu Gwajima, Silaa watiwa hatiani na Bunge

Shahidi (Gwajima) hakuitendea haki hakuwa na nidhamu, heshima na hata ujio wake katika kamati ulikuwa wa dharau na kejeli uliopitiliza,”amesema Kigua.
Mwisho.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments