Recent-Post

HAJI MANARA ANUSURIKA NA AJALI MBAYA YA GARI USIKU

BAADA ya jana, Yanga kukamilisha kilele cha Wiki ya Mwananchi, Ofisa Habari wao Haji Manara muda wa kurejea nyumbani anasema kuwa alipata ajali mbaya ya gari.

Manara ambaye aliibuka Yanga akitokea Simba leo alikuwa na mahojiano na kituo cha E FM jambo ambalo limemfanya akwame kufika katika kituo hicho kwa ajili ya mahojiano.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara aliweza kuwajibu E FM baada ya kuandika taarifa yenye kichwa cha habari, "Haji Haji'. 

Kupitia Ukurasa wake Rasmi wa Istagram, Manara ameandika:" Ndugu zangu EFM nawaomba radhi sana kwa kutofika kwenye kipindi asubuhi ya leo kama nilivyoahidi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.

Usiku wa jana nilinusirika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kuharibika vibaya gari yangu.

Hadi kuja kulala ilikuwa ni mida mibaya ya usiku mkubwa na sikuweza kuamka mapema ili niwahi kipindi chenu alfajiri ya leo saa kumi na Mbili.

Nawaomba tena radhi nyie na wasikilizaji na watazamaji wote. Mnisamehe sana na nimejisikia vibaya sana," .

Post a Comment

0 Comments