JEMBE JIPYA YANGA LINAWAZA MAKOMBE TU

  INGIZO jipya la Yanga limeweka wazi kwamba limekuja kujiunga na kikosi hicho ili kubeba mataji mengi kwa msimu wa 2021/22.Ni Bangala Litombo ambaye ni beki na inaelezwa kuwa dili ambalo amesaini ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ni miaka miwili.


Nyota huyo ambaye ni beki tayari ameshatambulishwa kwa Wananchi na ujumbe ambao walipewa ulikuwa ni kwamba sasa ni rasmi Bangala ni njano na kijani.


Beki huyo amesema: "Najua Yanga ni timu kubwa jambo ambalo lilifanga nikakubali kusaini hivyo uamuzi wangu upo sahihi na nipo mahali sahihi.


Kikubwa ambacho nahitaji kuona ni kwamba timu inapata matokea na kuweza kufikia mafanikio ambayo ni kutwaa makombe.


Timu kubwa inatwaa makombe ipo hivyo kwa Yanga hivyo tutapambana kufikia malengo,".

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments