Recent-Post

Kamati yaomba kibali cha kumkamata Silaa


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge,   Emmanuel Mwakasaka amesema ameomba kibali kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kukamatwa kwa mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa baada ya kutofika katika shauri lake.

Silaa alihojiwa mara ya kwanza na kamati hiyo Agosti 24, 2021 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Mwakasaka alimtaka kurudi tena leo Alhamisi kuendelea na mahojiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Agosti 26, 2021 mwenyekiti huyo amesema ameomba kibali cha kukamatwa kwa mbunge huyo baada ya kutofika katika shauli lake.

Mwakasaka amesema Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati hiyo ilimsubuiri hadi saa 8.00 mchana,  hivyo wamemwomba Spika kutoa kibali cha kukamatwa kwake na kufikishwa katika kikao cha kamati hiyo kesho saa 4.00 asubuhi.


Silaa pamoja na Josephat Gwajima Mbunge wa Kawe (CCM), waliitwa mbele ya Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.


Post a Comment

0 Comments