Recent-Post

LIVERPOOL WANAISAKA SAINI YA NAHODHA INSIGNE

Nyota wa kikosi cha Napoli ambeye ni nahodha pia Lorenzo Insigne aliyefanya vizuri katika EURO 2020 saini yake inagombaniwa na timu nyingi ikiwa ni pamoja na Liverpool, Everton ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.

Mbali na timu hizo pia Inter Milan ambayo inayoshiriki Serie A inaipigia hesabu saini ya nyota huyo ambaye ni mshambuliaji aliyeletwa duniani mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 30.

Raia huyo wa Italia ni moja ya nyota ambao wamekuwa wakitajwa sana kusepa ndania ya timu yake ya sasa inayoshiriki Serie A hivyo huenda atakuwa kwenye changamoto mpya dili lake likijibu.

Kwa upande wa Liverpool wao imeelezwa kuwa wanahitaji saini za wachezaji watatu kabla ya dirisha kufungwa huku miongoni mwa nyota wanaotajwa ni pamoja na Insigne pia Inter Milan wao wanasubiri dili lao kujibu kwa mshambuliaji huyo ambaye ni chaguo lao pia.

Post a Comment

0 Comments