Majaliwa akemea uonevu kwa watumishi


 Dodoma.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza waajiri nchini kuwapa nafasi ya kuwasikiliza watumishi kabla ya kuwapa hukumu.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumatano  Agosti 25, 2021 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) ambao pia utahusisha na uchaguzi mkuu wa viongozi.

Waziri Mkuu amesema hakuna haki kama mtu anatuhumiwa na hapewi nafasi ya kujieleza mbele ya anayemtuhumu na badala yake anapewa hukumu.

Ameagiza kila anayemtuhumiwa apewe nafasi ya kusikikizwa na kutokuwa na vielelezo isitumike kama fimbo ya kumwadhibu mhusika kwenye makosa yake.

"Lakini jambo la muhimu ni kutunza kumbukumbu za watumishi pamoja nanyi wafanyakazi muwe na kumbukumbu zenu ili wao wakikosa ninyi mnakuwa nazo," Amesema Majaliwa.

Kiongozi huyo meagiza haki kutendeka kwa watumishi ili kupunguza uonevu na malalamiko ambayo yamekuwa yakizidi mara kwa mara.

Amesema kwa upande wake Serikali katika kipindi cha miaka mitatu imeongeza Kasi ya usikilizaji wa rufaa za wafanyakazi na nyingi zimetolewa maamuzi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewaagiza waajiri kuwa tayari kuwarudisha majumbani kwao watumishi wanapokuwa wamestaafu kwani wengi wanakwama kutokana na kutolipwa nauli zao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments