Recent-Post

Manara awatoa hofu wasemaji Yanga


 Siku moja baada ya aliyekuwa msemaji wa Simba, Haji Manara kujiunga na klabu ya Yanga, amewahakikishia Antony Nugaz na Hassan Bumbuli kufanya nao kazi kwa pamoja lengo ni kuhakikisha Yanga inaikamata nchi.

Amesema baada ya kutambulishwa kumekuwa na mijadala mingi watu wakihoji ndugu zake Nugas na Bumbuli watafanya kazi gani.

“Nimekuja Yanga kufanya kazi niwahakikishie Bumbuli na ndugu yangu Nugaz mtafurahi kufanya kazi na mimi kuweni na amani tupo pamoja,” anasema na kuongeza kuwa.

“Hawa ni ndugu zangu nawafahamu sana hivyo tutaungana pamoja kufanya kazi bora ndani ya Yanga tutahakikisha inakuwa bora kila idara,” anasema.

Post a Comment

0 Comments