Mfanyabiashara maarufu Mtei afariki dunia

Mfanyabiashara maarufu mkoani Manyara, James Mtei ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Jambo Express amefariki dunia ghafla.

Awali, Mtei alikuwa mmoja kati ya wakurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Mtei, amefariki jana Jumanne Agosti 24, 2021 akiwa nyumbani kwake.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Agosti 25, 2021, Elly Mtei ndugu wa marehemu amesema kaka yake amefariki ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa nyumbani kwake.

Amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwake Mrara mjini Babati.

Baadhi ya ndugu wapo hapa mjini Babati kwa mipango ya taratibu za mazishi ili kupanga taratibu za siku na mahali maziko yatakapofanyika," amesema Mtei.

Mbunge mstaafu wa Jimbo la Babati Vijijini, Vrajilal Jituson amesema mji wa Babati na mkoa mzima wa Manyara, umepoteza mdau muhimu na maarufu wa maendeleo.

Jituson amesema wanamuombea marehemu Mtei apumzike kwa amani na jamii iige mazuri yote aliyofanya kipindi cha uhai wake.

Alikuwa ana utu mwenye kujitoa kwa hali na mali ikiwemo usafiri na huduma za jamii, michango ya ujenzi wa shule, zahanati na maendeleo mengine, Manyara tumepata pigo kubwa," amesema Jituson.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments