Mukoko, Kibwana, Yacouba wabeba tuzo Yanga

WACHEZAJI Tonombe Mukoko, Yacouba Songne na Shomari Kibwana kila mmoja amepewa tuzo na Sh3 milioni kila mmoja kama zawadi za kufanya vizuri msimu uliopita.

Mukoko amepewa zawadi hizo kama mchezaji bora wa Yanga wa msimu uliopita huku Yacouba akipiwa kama mfungaji bora wa timu kwa msimu uliopita na Kibwana kama mchezaji kijana bora wa Yanga kwa msimu uliopita.


 Watatu hao wamekabidhiwa zawadi hizo kabla ya kipindi cha pili cha mechi ya kirafiki kati ya Yanga na Zanaco kuanza katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Sambamba na hilo, Yanga wameingia katika kipindi cha pili na jezi nyingine za njano zenye dizaini tofauti na zile walizochezea kipindi cha kwanza za kijani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments