Nyumba 20 zateketea kwa moto Rufiji

Nyumba 20 zimeteketea kwa moto usiku wa jana Agosti 29 katika kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwara Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Abubakar Kunenge  amethibitisha tukio hilo na kusema ajali hiyo ilitokea saa 1.30 usiku kuamkia jana baada ya mwananchi mmoja katika eneo hilo kusafisha shamba lake kwa moto ambao ulimshinda nguvu na kusambaa na kuunguza nyumba hizo.

Kunenge ambaye usiku huo alifika eneo la tukio ili kuona athari halisi ya ajali hiyo amesema hakuna majeruhi yeyote katika tikio hilo  kwani wananchi waliokuwa wakiishi humo waliweza kutoka nje ya nyumba na kwamba wengi walipoteza mali zikiwemo nguo.

Kufuatia tukio hilo, Kunenge ameagiza wanafunzi wote katika eneo hilo waruhusiwe kwenda shuleni bila sare.

Pia ameelekeza wananchi wote wenye maeneo yenye nyasi wasafishe maeneo yao kuondoa nyasi zinazozunguka makazi yao ili kuepusha madhara mengine kama hayo kujirudia
"Nimefika nikiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya  nimeona  madhara, natoa pole kwa serikali ya wilaya na pamoja na wananchi waliokutwa na madhira hayo na pia nawapongeza wakazi  wa karibu kuwapatia hifadhi wenzao," amesema Kunenge.

Ameiagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya tathimini haraka kujua athari iliyopatikana ili kuweza kuwasaidia waliopata adhari kwa tukio hilo.

Mkuu wa wilaya hiyo Meja Edward Gowele amewataka wananchi kwa ujumla wa wilaya hiyo kuacha tabia ya kuchoma nyasi nyakati hizi ambapo ni kipindi cha upepo mkali.

Mmoja wa wakazi waliounguliwa nyumba, Ally Manjula amesema moto umetokea kati ya saa saba na nane usiku muda ambao kulikuwana upepo mkali na hivyo kuchochea moto kusambaa kwa kasi.

Naye Mariamu Saidi ameongeza kuwa walikua wamelala na aliposhtuka waliona moshi mkubwa umetanda na moto ulikua ukichochewa na upepo mkali ulioku mkali ukivuma usiku.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments