Pombe ya Mkobola yalalamikiwa kupunguza nguvu za kiume

Baadhi ya kina mama katika Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma wamelalamika waume zao kuishiwa nguvu za kiume kutokana na matumizi ya pombe aina ya Mkobola.

Kutokana na athari zinazosababishwa na pombe hiyo, ikiwamo wanywaji kujisaidia haja kubwa na ndogo kwenye nguo na kudhoofu afya zao, kina mama hao wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kuifanyia vipimo pombe hiyo kama inafaa kwa matumizi ya binadamu.

Pombe hiyo inayoelezwa ni maarufu kwenye vijiji vya Majengo, Hazina na Ilolo imewafanya vijana wa kiume kutofanya kazi kutokana na kuwa dhaifu. Mmoja wa akina mama katika Kijiji cha Ilolo aliyejitambulisha kwa jina la Sikitu Samina alisema: “Ukweli mwandishi tumeamua kutafuta watu wa kutuliwaza kutokana na shida hii kukua siku hadi siku, wanaume zetu hawashikiki na hawawajibiki kwa lolote, ikiwemo haki ya msingi ya faragha,” alisema Sikitu.

Alisema kutokana na ulevi wa pombe hiyo, migogoro ndani ya nyumba imekuwa mingi na kuathiri watoto kisaikolojia kwa sababu baadhi ya wanaume walioathirika na pombe hiyo hawafanyi shughuli za kujiingizia kipato na hawawaridhishi wake zao pia.

Mwanzo nilijua mume wangu amepata mwanamke mwingine, kumbe pombe hiyo imemwathiri, yaani hakuna kitu kabisa tunalala kama dada na kaka,” alisena na kuongeza:

Mwandishi mimi ni binadamu na mwili ukipata njaa utakula ugali, sasa haki za msingi nitazipata wapi, inabidi nijiongeze, naenda kijiji cha pili natafuta mtu atakaenisitiri, basi maisha yanakwenda hivyo,” alilalamika Sikitu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments