Recent-Post

Samatta atua Ubelgiji kujiunga na Royal Antwerp

 

NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ametua leo, Jumanne huko Ubelgiji ikiwa ni siku ya mwisho ya usajili barani Ulaya kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na  Royal Antwerp akitokea Fenerbahce ya Uturuki.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Samatta, Jeff Megan ambaye  makazi yake yapo Ubelgiji, ametuthibitishia taarifa hiyo kwa kusema Antwerp wamempa ofa nzuri zaidi.

"Ametua leo Ubelgiji majira ya mchana hivi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, baada ya hapo nadhani atajiunga na timu ya  taifa kwa ajili ya michezo ya kufuzu  kombe la Dunia,"

"Sio mbaya kurudi kwake Ubelgiji sehemu ambayo amejijengea jina kubwa, inawezekana akafanya tena makubwa kama ilivyokuwa wakati akiwa na  Genk  kwa sababu hii ni ligi ambayo anaifahamu," alisema.

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania uhamisho wake umeigharimu Antwerp kitita cha Euro 4milion ambazo ni zaidi ya Sh. 10.9 Bilioni.

Katika vita ya kuiwania saini yake,Antwerp imepigana vikumbo  na klabu kadhaa ikiwemo Troyes na Montpellier za Ligi Kuu Ufaransa.Montpellier iliweka mezani Euro 2.5milioni. Kupigwa bei kwa Samatta kumefungua milango kwa Fenerbahce kumnasa Stéphane Bahoken wa Angers kama mrithi wake.


Post a Comment

0 Comments