Serikali imelipa madai ya mabilioni kwa waliorejeshwa kazini

Serikali ya Tanzania imelipa madai ya mishahara ya jumla ya Sh2.61bilioni kwa watumishi 1,643 waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Agosti 31 2021 na Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mikumi (CCM) Denis Londo.

Mbunge huyo amehoji ni watumishi wangapi wamerejeshwa kazini baada ya kuondolewa kimakosa wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti feki na wafanyakazi hewa.

Watumishi wangapi waliorejeshwa kazini wamelipwa stahiki zao kama Mishahara ambayo hawakupata kutokana na kuondolewa kimakosa?” amehoji Londo.

Akijibu swali hilo, Ndejembi amesema imelipa madai ya mishahara ya jumla ya Sh2.61bilioni kwa watumishi 1,643 waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa.

Amesema zoezi la uhakiki wa madai yaliyobaki unaendelea na yataendelea kulipwa kwa kadri yanavyohakikiwa.

Akifafanua zaidi amesema Serikali imewarejesha kazini watumishi imewarejesha kazini na kuendelea kuwalipa mishahara watumishi 4,380 walioondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti vya elimu na watumishi hewa.


Amesema idadi hii inajumuisha watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na watendaji wa mitaa wapatao 3,114.

Amesema Serikali pia ilitoa msamaha wa kuwarejesha kazini watumishi walioondolewa kazini kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne na baadaye wakajiendeleza na kupata sifa tajwa hadi kufikia Disemba, 2020.

Hata hivyo, amesema msamaha huo ulitolewa kwa watumishi ambao hawakudanganya katika taarifa zao kuwa wana elimu ya kidato cha nne au kubainika kughushi vyeti.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments