SERIKALI MKOANI SINGIDA IMEWAKARIBISHA WADAU KUJA KUWEKEZA KUTOKANA NA MKOA HUO KUWA NA UMEME MWINGI UNAOBAKI BAADA YA MATUMIZI


Imeelezwa kuwa mkoa huo unapokea umeme megawatt 232 wakati matumizi halisi kwa sasa ni megawatt 10 pekee,hivyo zaidi ya megawatt 220 zinabaki bila matumizi

Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano maalumu wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya Singida Mjini wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi mwaka 2015,2020

Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskas Muragiri pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kwakuwakaribisha wadau mbalimbali kuja kuwekeza mkoani hapa kwani nishati ya umeme ni ya uhakika

Kwa upande wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Ilani amewahakikishia wajumbe kuzitatua changamoto hizo kwa kuwaagiza Viongozi wa sekta na Idara mbalimbali za Manispaa kwenda kusimamia ipavyo huku wakitafuta njia za kumaliza changamoto chache zilizojitokeza.

Baada ya wajumbe hao kuipokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya Lucia Mwiru aliwataka wakuu wa Idara kuhakikisha zile kasoro chache zizojitokeza zinatatuliwa mapema kwa maslahi ya wananchi ili pia wananchi waendelee kukiamini chama hicho
        
           Na Revocatusi Phiniasi :Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments