Sir Alex afanya umafia, amrudisha CR7 Man United


MANCHESTER, ENGLAND. MAMBO yanakwenda haraka sana. Ghafla tu, Cristiano Ronaldo amebadili mawazo akiachana na mpango wa kujiunga na Manchester City na kutua Manchester United.

Kinachoelezwa ni kwamba umefanyika umafia mkubwa katika kumfanya Ronaldo agome kwenda Etihad na kurudi zake Old Trafford, ambapo Sir Alex Ferguson alidaiwa kuzungumza na fowadi huyo kwa simu asubuhi ya jana Ijumaa na kubadili kila kitu. Baadaye Man City walitangaza kujitoa kwenye dili hilo.

Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer alisema: "Sidhani kama Cristiano ataondoka Juventus. Lakini, kama atakuwa anaondoka Juventus, anafahamu sisi tupo. Siku zote tumekuwa na mawasiliano mazuri sana, Bruno Fernandes amekuwa akizungumza naye pia. Anafahamu hisia zetu kwake. Ni gwiji kwenye klabu, ni mchezaji bora wa nyakati zote, hivyo subiri tuone kitakachotokea."

Beki wa kati wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand alithibirisha kuzungumza na Ronaldo kwa simu, akimuuza Mreno huyo kipi kinaendelea kabla ya kutumia ukurasa wake wa Twitter kudai dili la kwenda Etihad limekufa na mchezaji huyo anatua Old Trafford.

Ronaldo ametua Man United kwa ada ya Pauni 24 milioni huku akiripotiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mshahara wa Pauni 480,000 kwa wiki.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema: "Ninachoweza kusema zimebaki siku tatu au nne, chochote kinaweza kutokea. Lakini, kwa mtazamo wangu ni wachezaji wachache sana, Ronaldo na Messi ndio wanaoamua wapi wakacheze. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments