Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua jengo jipya la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida leo. Wengine kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christopher Kadio.
(Picha zote Dotto Mwaibale na Godwin Myovela)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.Muonekano wa jengo hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua jengo la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Singida. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Stella Rutabihirwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Salamu ya Mkuu iliyoambatana na Wimbo wa Taifa kutoka 'Mounted Guard' ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Singida muda mfupi alipowasili Makao Makuu ya Kikosi hicho mkoani hapa kwa shughuli ya kuzindua moja ya jengo lake.
Askari wa FFU wakiwa kwenye maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kuwasili kuzindua jengo jipya la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
Afisa Mwandamizi kutoka Kampuni ya Biosustain mkoani Singida Abdulazizi Chaudhry na Wadau wengine mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo akiteta jambo na Mbunge wa Manyoni Mashariki Dkt.Pius Chaya.
Singida Na Doto Mwaibale
0 Comments