Licha ya kufanya vitu kadha wa kadha kulinda ngozi isiharibike, kuna sababu za kimaumbile, ikiwamo mabadiliko ya homoni ambayo huifanya ngozi kubadilika na wakati mwingine kupata chunusi.
Soma hapa: Mambo gani wanawake watarajie wanapokaribia kukoma hedhi
Hili hutokea kwa baadhi ya wanawake kila mwezi wanapokuwa kwenye hedhi. Ili kukabiliana na hali hii, unapaswa kuhakikisha unajua tarehe unazopata hedhi. Ukijua tarehe za kupata hedhi, zikikaribia
kanda uso kwa mvuke.
Yaani chemsha maji yaweke kwenye chombo kipana kama beseni kisha jifunike nguo nyepesi ili kupata mvuke,
Soma hapa: Fahamu mzunguko sahihi kwa mwezi
hakikisha hayana moto sana ili kuepuka kubabuka. Kama una mashine ya mvuke unaweza kuitumia, mara nyingi zinakuwepo kwenye saluni za kiume.
Ikiwezekana pia osha uso mara mbili kwa siku kwa sabuni unayoitumia, pia usilale na vipodozi na ukiweza punguza kutumia vyenye mafuta.
0 Comments