Recent-Post

Aliyemfumua mshono mgonjwa kwa kushindwa kulipia gharama asakwa

Wizara ya afya nchini Tanzania imeeleza masikitiko yake kuhusu mtaalam mmoja wa afya aliyemshona mgonjwa jeraha  na kisha kulifumua kwa madai kuwa hakuweza kulipa gharama.

Video ya mtaalam huyo ambaye kituo chake cha afya hakijafahamika imesambaa mitandaoni na kuibua hali ya sintofahamu jambo ambalo wizara hiyo imelitolea tamko leo Jumamosi Septemba 4, 2021.

"Ikiwa hili limetokea nchini basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu. Hivyo, wizara inaomba wenye taarifa za wapi  au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya wizara ya afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya waziri wa afya ya 0734124191, " inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments