Recent-Post

AZAM FC KAMILI GADO KUIVAA COASTAL UNION

 

UONGOZI wa Azam FC umebainisha kuwa unahitaji pointi tatu kesho mbele ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani. 

Tayari kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kimeshatia timu mapema Tanga ilikuwa jana Septemba 25 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amebainisha kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kuanza vema ligi licha ya kwamba mchezo huo utakuwa mgumu.

"Tupo tayari kwa ajili ya ligi na tunatambua kwamba mchezo wetu wa kwanza itakuwa ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga pale Mkwakwani, hakuna namna ni lazima tupambane ili kufanya vizuri na inawezekana,".

Msimu uliopita Azam FC ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu na pointi 68 inakwenda kukutana na Coastal Union iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya 13 na pointi 40 kwa msimu wa 2020/21.

Post a Comment

0 Comments