Recent-Post

Baba mbaroni kwa kisa cha 'aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake'

LAGOS, Jeshi la Polisi katika Jimbo la Nigeria la Lagos limemtia mbaroni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka minane kwa kutumia jiwe la moto.

Rekodi ya polisi inaonyesha kuwa, baba huyo alitekeleza maasi dhidi ya binti yake, kwa sababu matiti yake yalikuwa yameanza kuonyesha 'chuchu', ambazo ni ishara za kwanza za kubalehe.

Kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko katika hali mahututi, kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi Bwana Banjo.

Baba yake msichana huyo aliripotiwa polisi na kikundi cha kutetea haki za watoto, na Msemaji wa polisi wa jimbo la Lagos, DSP Asijebotu amethibitisha madai hayo, akisema kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa nchini Nigeria, wazazi wa msichana huyo kwa sasa wanashikiliwa na polisi katika jimbo la Lagos.

Mkuu wa Kikundi cha Kutetea Haki za Watoto, Comrade Ebenezer Omejalile, ambacho kilimshitaki baba huyo, ameiambia BBC kwamba, Bwana Banjo, anayefahamika kama Panel, "Aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake."

"Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake," alisema.

Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake, na ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.

Aidha, Mama yake msichana huyo alisema kuwa mumewe amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara. (BBC).

Post a Comment

0 Comments