CCM BAGAMOYO YATOA MAAGIZO KWA HALMASHAURI, WATENDAJI

 


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM ), Wilaya ya Bagamoyo ,mkoani Pwani, kimeiagiza ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo na watendaji wake ,kuhakikisha wanatolea majibu na kutatua changamoto za muda mrefu zinazotolewa na madiwani bila majibu.

Aidha kimetaka wataalamu kushirikiana na madiwani na kujenga mahusiano mazuri ili kuimarisha mahusiano mazuri katika utendaji kazi wao.

Katibu wa CCM Bagamoyo, Getruda Sinyinza alitoa maagizo hayo wakati wa kikao Cha madiwani Bagamoyo,Chenye ajenda kuu kuwasilisha taarifa za kata kwa kata.

Alisema ,zipo changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri na wataalamu ambazo zinapaswa kutekelezwa kwa haraka pasipo kukaa nazo na kujikumbusha kila kikao kwa kipindi kirefu .

"Madiwani hawa wanatoa taarifa hizi kutoka kwa wananchi ,,hawazitoi kichwani mwao , hivyo zinahitaji matokeo ,;"Ili tunusuru wananchi hawa tunaomba mambo yote mkayafanyie kazi ,na changamoto zisizo na majibu zisemwe pasipo kukaa kimya" alifafanua Getruda.

Kwa upande wake ,mwenezi wa Wilaya (CCM) ,John Fransis Bolizozo aliwaasa , watumishi na watendaji wapige kazi waache kufanya kazi kwa mazoea .

"Tufanyeni kazi ,tunamsaidie Rais na mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ,Samia Suluhu kuyaeleza yote yanayofanywa na serikali na ambayo yapo katika hatua za utekelezaji ili kuondoa maswali kwa jamii.'"alibainisha Bolizozo.

Nae mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo , Mohammed Usinga akipokea maelekezo hayo ,alimtaka mkurugenzi na timu yake kupeleka watumishi wa kukusanya mapato katika chanzo Cha mchanga na mazao ya matunda kata ya Fukayosi.

Alieleza, halmashauri ipo kwa ajili ya kulenga kuongeza mapato ,hajaridhishwa kusikia kuna changamoto ya ukosefu wa watumishi hao .

Usinga pia alielekeza ,, mkurugenzi na Bwana fedha kuhakikisha fedha asilimia 10 ,fedha za vibarua na za wazabuni wa makusanyo zinapelekwa kwa wakati.

"Wanatufanyia kazi nzuri ,kwenye wastani wa milioni kumi sasa tumefikia zaidi ya milioni 20,tusicheleweshe fedha zao itasababisha upenyo wa wizi"anasema Usinga.

Awali ,akiwakilishwa diwani wa Fukayosi,Ally Ally Issa taarifa yake ya kata ,imeweka bayana tatizo la ukosefu wa watumishi wa kukusanya mapato kwenye chanzo Cha mchanga na mazao ya matunda.



                                Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments