CCM KUWEKA MISINGI MADHUBUTI KUENDELEZA SANAA NCHINI

Akizungumza kupitia jukwaa  la wasanii liloandaliwa na kampuni ya Marketing Africa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka amesema serikali ya CCM itaendelea kuweka misingi Imara ya kuendeleza Sanaa nchini.


Aidha Shaka ameleza kuwa  dhamira njema kabisa ya kukuza na kuwathamini wasanii, Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanzisha Wizara Maalum ya Sanaa na Utamaduni lengo likiwa  ni  kushughulikia changamoto za wasanii zilizopigiiwa kelele kwa muda mrefu.

Kwa kupitia Hotuba ya Mhe Rais ya Baraza kuu la umoja wa mataifa, suala la sanaa sasa litachukua mkondo mpya katika uwanja mpana wa kimataifa, kushirikiana na wasanii wengine wa dunia katika uwekezaji mku
bwa katika sanaa kupitia sera yetu ya deplomasia ya uchumi.


"Tuitumie sanaa kama  Silaha ya ukombozi wa matatizo ya kijamii na kamwe isiwe chanzo cha mfarakano na vurugu" amesema Shaka

Aidha ameendelea kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi Tajiri, yenye rasilimali za kila aina, na rasilimali namba moja ni vipaji tulivyonavyo  hivyo Wasanii wakiamua wataweza , kila mmoja wetu ana jukumu la kufanya sanaa yake kwa bidii na maarifa. Na huu ni wakati wa Suluhu, hivyo wasanii wawe wazi kuacha kufanya sanaa kwa mazoea.

 "Katika   Zama tulizonazo, kazi ya sanaa imegeuka kuwa kimbilio kubwa kwa vijana kama sehemu ya soko la ajira hivyo ni wajibu  wetu wasanii kuhakikisha kuwa imani ya Jamii kwetu inaendelea kwa kulinda mila, desturi na utamaduni wetu." Amesema Shaka

Jukwaa ili limeandaliwa kwa lengo la kutoa elimu ya masoko, uzalishaji bora wa kazi sanaa sambamba na kutoa ushauri wa kibiashara.
 









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments