Recent-Post

CCM yampitisha Msuya kugombea Udiwani Kileo Mwanga


 Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro imempitisha Kuria Msuya kugombea Udiwani wa kata ya Kileo wilaya ya Mwanga katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Oktoba 9, 2021. 

Kata ya Kileo imeingia katika uchaguzi wa marudio, baada ya aliyekuwa Diwani wake Salimu Zuberi (CCM) kufariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake, Katibu wa Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya amesema, wajumbe wa kikao hicho pamoja na kujadili mambo mengine pia walijadili kushinda chaguzi zote za marudio zitakazotokea. 

Amesema mchakato wa awali wa ndani ya chama kutoa fomu kwa wanachama wake kuomba ridhaa ya kugombea ulifanyika Septemba 5 na 6 mwaka huu ambapo jumla ya wanachama 9 walichukua fomu. 

"Baada ya tarehe ya uteuzi ya tume kukamilika Septemba 19 chama kinatarajia kuzindua kampeni zake Septemba 20 mwaka huu na tunaamini tutashinda kwa kuwa tumemsimamisha mtu sahihi", amesema Mabihya.

Mkoa wa Kilimanjaro una jumla ya kata 169, ambapo katika uchaguzi mkuu 2020, CCM ilishinda kata 168 huku chadema ikishinda kata moja.

                                                           Moshi

Post a Comment

0 Comments