DIWANI KATA YA LIWITI KUSIMAMIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI

DIWANI wa Kata ya Liwiti wilayani Ilala jiijini Dar es Salaam  Alice Mwangomo anatarajia kusimamia ujenzi wa Shule ya Sekondari   ya Serikali ambayo ujenzi wake unaanza hivi karibuni.


Shule ya sekondari hiyo inajengwa kwa fedha za Serikali ili kuwapunguzia adha Wanafunzi wa sekondari waliokuwa wakisoma shule za mbali miaka yote.

" Serikali imetoa fedha shilingi milioni 420 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya sekondari Kata yetu ambayo itakuwa ya ghorofa na ujenzi utakamilika Januari 2022, "ameema Alice.

Ameongeza kuwa  mwaka 2022 wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kusoma katika shule yao mpya hii yote ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Alice amesema kukamilika kwa shule hiyo ya sekondari itapunguza adha ya Wanafunzi ambao waliokuwa wakifaulu ndani ya Kata hiyo wanapangiwa shule za mbali .

Pa ujenzi huo Halmashauri wamechangia Sh.milioni 120 na Serikali Kuu Sh. milioni 300."Ujenzi wa Shule hiyo ya sekondari utatoa fursa mbalimbali kwa vibarua na mama lishe wote watapewa ajira kutoka ndani ya Kata hiyo."

Kwa upande wake Ofisa Elimu  Sekondari Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally aliagiza kamati za ujenzi kushirikiana na Ofisa Elimu Kata na Wilaya katika kusimamia ujenzi wa Shule hiyo mpaka unamalizika.

Ofisa Elimu Mussa amesema hiyo ni fedha ya Serikali imetolewa hiyo Kamati ya ujenzi isimamie kwa weledi kwa ushirikiano na DIWANI wa Kata  na ujenzi huo utakuwa wa( Fosi  akaunti)

 Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, ambaye aliwakilishwa na Katibu wake Lutta Rucharaba, amesema atahakikisha mipango yote iliyopangwa kwa ajili ya ujenzi huo inakamilika mapema ili watoto waanze kusoma Januari mwakani.

Amesema Jimbo la Segerea kwa sasa lina shule 17 za sekondari na kati ya hizo sita zimejengwa kati ya mwaka 2016 na 2021 chini ya uongozi wa mbunge huyo.

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Steven Mushi, amesema sambamba na ujenzi wa shule hiyo pia wamepanga kukarabati vyumba vya madarasa katika shule mbili za msingi zilizopo kwenye kata hiyo ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.

Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangomo akizungumza na wananchi wake kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari itakayojengwa katika kata hiyo
Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangomo(kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii   Halmashauri ya Jiji La Dar es Salaam Steven Mushi.
Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangomo akisalimiana na Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally wakati wa kikao cha wananchi cha sekta ya Elimu.
                            Na Heri Shaban

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments