Recent-Post

DKT. MAHENGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANYONI AWAPONGEZA WANANCHI

 

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Zahanati  ya Kijiji cha Maweni wilayani  Manyoni katika  Hafla iliyofanyika kijijini hapo jana wakati wa zaira yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Wengine ni viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa  akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi vifaa vijana Wajasriamali walivyowezeshwa na Shirika la Compassion International Tanzania (CIT)

Meneja wa Shirika la Compassion International Tanzania (CIT) Kanda ya Kati Emmanuel Pando akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi  vifaa hivyo.
Askofu Elisante Mwenegoha wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge akiangalia baadhi ya vifaa waliokabidhiwa vijana hao na Shirika la Compassion International Tanzania (CIT)
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedek Humbe akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati ya kijiji cha Maweni.
Vijana wanufaika wa msaada huo wakiwa kwenye hafla hiyo. 
Wananchi wa Kijiji cha Maweni wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Maweni wakiwa kwenye hafla hiyo.


Dkt. Mahenge akimkabidhi Kadi ya Bima ya Afya iCHF iliyoboreshwa Mzee Godwin Nguluga.

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dkt. Pius Chaya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni Jumanne Muhanda akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wakiwa kwenye hafla hiyo.

Makabidhiano yakiendelea.

Makabidhiano yakiendelea.

Vijana wanufaika wa msaada wa vifaa hivyo Shukrani Leonard na Asha Kidaga wakisoma risala mbele ya mkuu wa mkoa.

Makabidhiano yakiendelea.

Makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakimsikiliza mkuu wa mkoa (hayupo pichani) 
Wanafunzi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Ukaguzi wa Zahanati ya Maweni ukiendelea.
 

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Maweni kilichopo wilayani Manyoni mkoani hapa kwa hatua walioichukua ya ujenzi wa Zahanati ambayo inakwenda kuondoa adha waliyokuwa wakiipata kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu maeneo ya mbali.


Dkt. Mahenge ametoa pongezi hizo jana wakati akikagua miradi ya maendeleo wilayani Manyoni mkoani hapa leo ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na wananchi.

"Hatua yenu mliyoichukua ya  kuhamasishana na kupata Sh. 9 Milioni kwa ajili ya kuanza ujenzi huu na kuungwa mkono na Serikali hadi kukamilisha ujenzi wa zahanati hii mnastahili kupongezwa naomba na vijiji vingine viige mfano huu,". alisema Mahenge.

Dkt. Mahenge alitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wa chama na Serikali kwa wa wilaya hiyo kwa kufanikisha kukamilisha ujenzi huo.

Mganga Mkuu wa hiyo Furaha Mwakafwila akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo alisema itahudumia wakazi wa kijiji hicho 3749 ambao wanaizunguka na kuwa gharaza zote za kukamilisha ujenzi huo umegharimu zaidi ya Sh. 82 Milioni.

Akizungumzia kuhusu watumishi watakao kuwa wakitoa huduma kwa wananchi katika zahanati hiyo kwa maana waganga na wauguzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Melkizedek Humbe alisema tayari wamepatikana na mmoja atafika hivi karibuni baada ya kumaliza masomo yake mwezi huu kwa ajili ya kumsaidia aliopo wakiwepo wahudumu wa afya ya jamii ambao wametakiwa kufika kuongeza nguvu ya kuhudumia wananchi. 

Alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha unaokuja watatenga fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa majengo mengine ya zahanati hiyo.

Katika hatua nyingine Dkt.Mahenge alilipongeza Shirika la Compassion International Tanzania  (CIT) kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali kutoka vikundi vituo vinne vya huduma ya mtoto na kijana Klasta wilayani humo kwa kuwapa vifaa mbalimbali vya uzalishaji mali vyenye thamani ya zaidi ya Sh.80. 4 Milioni.

Vikundi hivyo ni kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT), Kanisa la Moravian, Kanisa la Evangelist Assemblies of Gof (EAGT) na Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)

Meneja wa Shirika hilo Kanda ya Kati,  Emmanuel Pando alisema shirika la CIT limekuwa likitoa fedha za ufadhili sio chini ya Sh. 1.4 Bilioni kila mwaka kwa makanisa 10 ya Klasta ya Manyoni na kwa miaka 15 makanisa yamepokea takribani Sh. 18 Bilioni kwa ajili ya kuwahudumia watoto na vijana.

Alisema lengo la shirika hilo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha vijana kiuchumi na kutatua changamoto ya ajira.

Afisa Vijana  Mkoa wa Singida Frederick Ndahani pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuzindua mradi wa vijana hao na kuwakabidhi vitendea kazi mbalimbali vikiwemo pikipiki  na mizinga vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. 80.4 Bilioni  amezishukuru Taasisi za dini kwa kuwajali na kuwasaidia vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

Katika ziara hiyo Dkt.Mahenge alitembelea Zahanati ya Kijiji cha Maweni na kuizindua, Alizindua vifaa vilivyotolewa na Shirika la CIT kwa vijana wa Klasta, Alikagua ujenzi wa madarasa matatu, Ofisi ya Mwalimu Mkuu na matundu nane ya choo cha Shule ya Msingi Sayuni pamoja na madarasa mawili Shule ya Sekondari Mlewa.
Na Dotto Mwaibale, Manyoni.

Post a Comment

0 Comments