FURAHA YA USHINDI WA YANGA DHIDI YA SIMBA WASABABISHA KIFO CHA POLISI

USHINDI walioupata Klabu ya Yanga wa bao 1-0 dhidi ya Klabu ya Simba na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa Ngao ya Jamii umesababisha kifo cha askari H.2636 Rashid Mohamed Jumaa.

Askari huyo alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na inaelezwa alifariki dunia saa 12 jioni alipokiwa akiangalia mtangane wa watani wa jadi Simba na Yanga maeneo ya Stendi ya basi ya Wilaya ya Mpwapwa.

Mtangane huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa mkoani Dar es Salaam ulikuwa ukioneshwa Live na kituo cha Luninga cha Azam TV ambao ndio waliopewa jukumu la kuonesha mechi za Ligi Kuu nchini.

Wakati akishangalia na kuwa na furaha iliyopitiloza askari polisi huyo alianguka chini,hivyo alichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ambapo baada ya kufikishwa hapo madaktari walithibitisha alishafariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa inayoelezea tukio cha kifo cha askari huyo inadai alikuwa shabiki wa kutupwa wa Yanga na ushindi wa bao 1- 0 ambaoYanga waliupata katika dakika ya 11 ya mchezo huo uliochezwa jana Septemba 25 mwaka huu 2021 kuanzia saa 11 jioni ndio unaodaiwa kusababisha kifo hicho.

Askari huyo aliyekuwa akifanya kazi katika Wilaya ya Mpwampwa ni mwenyeji wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

  Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments