Recent-Post

Hamisa na Fahyvanny ni pacha katika kazi na mapenzi


Hamisa Mobetto na Fahyvanny hawa ni wakali zaidi upande wa mitindo, kutokana na ubora wa kazi zao wamejikuta wakishinda tuzo mbalimbali za kimataifa na kujitengenezea upekee wao Bongo kama pacha.

Hivi karibuni wawili hao wameshinda tuzo za Scream 2021 kutoka Nigeria ambazo hutolewa kwa vijana barani Afrika waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali, huu ukiwa ni msimu wake wa nne kutolewa.

Hamisa ameshinda katika kipengele cha ‘Mshawishi Bora Chapa ya Mwaka’ (Brand Influencer of the Year), wakati Fahyvanny akishinda nafasi ya ‘Mshawishi Bora katika Mitandao (Social Media Influencer).

Ni wazi Hamisa ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa na dili nyingi za ubalozi kutoka kampuni mbalimbali, huku Fahyvanny akisifika kwa kuchapisha picha zenye mvuto kwenye ukurasa wake Instagram wenye wafuasi milioni 3 kwa lengo la kutangaza biashara yake ya nguo, maarufu ‘Fahyma Love Styles’.

Hizi ni tuzo za pili kushinda pamoja, awali kwa nyakati tofauti walishinda tuzo za Starqt zinazohusisha biashara, mitindo, michezo na burudani kutoka Afrika Kusini. Tuzo hizi zilizoanzishwa mwaka 2014 ni maalumu kwa huwatunuku mastaa wa Afrika kwa kazi wanazofanya katika sekta ya burudani na michez

Katika tuzo hizi Hamisa amewahi kushinda katika kipengele cha chaguo la watu na Fahyvanny akishinda kipengele cha mwanamke aliyependeza.

Ndiyo, pacha wanaofanana!, kwani Hamisa amewahi kutokea kwenye video ya mzazi mwenziye, Diamond Platnumz ‘Salome’ kama video vixen na Fahyvanny amefanya hivyohivyo kwa mzazi mwenziye, Rayvanny kwa kutokea kwenye video zake tatu, ‘Kwetu’, ‘Natafuta Kiki’ na ‘Safari’.

Utakumbuka wakati huu ambapo Rayavanny ameweka wazi yupo kati mahusiano na Paula, Fahyvanny bado anasema hana mtu (single), pia Hamisa tangu kujaliwa mtoto na Diamond amekuwa ni mtu wa kuweka usiri mkubwa katika mahusiano yake na wakati mwingine akisema hana mtu kabisa, wakati Diamond alishakuwa na Tanasha hadi wakaja kuachana wakiwa tayari na mtoto.

Hamisa pcc

Post a Comment

0 Comments